Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, jana Juni 24, 2014
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo leo Juni 24, 2014
kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa – African Union (AU).
Akiwa Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira. Rais Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
24 Juni, 2014


0 comments:
Post a Comment