Akizungumza katika kipindi chakili break fast show, Meneja wa
huduma za kibenki toka Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Boaz amesema
wameamua kubadili matumizi ya noti ya shilingi 500 na kutumia sarafu kwa
kuwa noti hiyo inachakaa haraka na mzunguko wake ni mkubwa sana kiasi
kwamba hairudi benki.
“Noti ya shilingi 500 kwa wasitani hushikwa na watu zaidi ya milioni
moja kwa siku. Na kwa wasitani tunaweza kusema noti moja hushikwa na
watu 20 hadi 25 kwa siku. Huo ni mzunguko mkubwa ukilinganisha na idadi
ya watu wanaoshika noti ya shilingi 10,000. ” Amesema Emmanuel Boaz.
“Na ukizingatia watu wengi wanaoishika noti hii ni wale wenye
matumizi ya kawaida ya nyumbani ambao wengi wao sio wanaopeleka benki,
hivyo noti hii kwa kiasi kikubwa hairudi benki, labda wanaorudisha benki
ni taasisi kama makanisa, misikiti n.k” Ameongeza.
Boaz amewatoa wasiwasi watanzania ambao wanadhani matumizi ya sarafu
hiyo yataleta madhara hasi kwa uchumi wa Taifa na kueleza kuwa
hakutakuwa na athari yoyote na kwamba tofauti na noti sarafu hiyo ina
uwezo wa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.
Sarafu hiyo itakayoanza kutumika rasmi miezi miwili au mitatu ijayo
ina taswira ya rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Sheikh Amani Abeid Karume.
0 comments:
Post a Comment