Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika hujuma za ndege za
kivita za utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo lililozingirwa la
Ukanda wa Ghaza imeongezeka na kufika zaidi ya 35.
Ripoti za hivi punde zinasema kwa uchache Wapalestina saba, wengi wao
wakiwa wanawake na watoto, wameuawa shahidi katika hujuma ya utawala
haramu wa Israel leo Jumatano na hivyo kuongeza idadi ya waliouawa tokea
Jumanne kufika 35.
Walioshuhudia wanasema ndege za kivita za Israel zimelenga majengo kadhaa ya makazi ya raia wasio na hatia. Karibu Wapalestina 300 wamejeruhiwa katika hujuma hizo za Israel ambazo zimelaaniwa kimataifa. Duru za habari zinadokeza kuwa hivi sasa utawala haramu wa Israel unapanga kufanya hujuma ya nchi kavu dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham amelaani mashambulizi makubwa ya Israel katika Ukanda wa Ghaza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Afkham amesifu mapambano ya raia shupavu wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza dhidi ya mashambulizi ya Israel. Aidha ametoa wito kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu na pia taasisi na makundi ya kutetea haki za binadamu kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya mauaji na jinai za utawala wa Kizayuni.

0 comments:
Post a Comment