Wednesday, July 9, 2014

Lil Wayne na Drake kufanya tour ya pamoja ya ushindani

Lil Wayne na Drake kufanya tour ya pamoja ya ushindaniRapper Lil Wayne ambaye ni boss wa Drake ameeleza kuwa hivi karibuni mashabiki wasubiri kuona tour yao ya pamoja ya ushindani.
Weezy ameeleza hayo wakati anazungumza na MTV katika utengenezaji wa video ya wimbo wake ‘Krazy’ ambapo alidai kutakuwa na battle kati yao kwenye majukaa mbalimbali watakapokuwa wakizunguka.
Amesema huo ulikuwa mpango wao tangu zamani kwa kuwa mara nyingi walipokuwa wakifanya shows pamoja walikuwa wanaona umati ukishangweka kwa hits zao kadhaa walipokuwa wakipokezana.
“I think it’s something like…it’s a battle tyepe thing.” Lil Wayne alifafanua.
Ziara ya Drake na Lil Wayne inatarajiwa kuanza August 8 Darien Center, New York kabla hawajaanza kuizunguka Marekani.
Katika hatua nyingine, rapper huyo alielezea kuhusu ujio wa albam yake mpya ya ‘The Carter V’ inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake. Alisema albam hiyo itakuwa na wasanii kadhaa wakiwemo Drake na Nicki Minaj kutoka Young Money.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...