Muimbaji Robin Thicke anazidi kukutwa na majanga zaidi baada ya
kumsaliti mkewe Paul, kosa lililopelekea kutoswa na mke wake. Sasa
albam nzima aliyoiimba kwa ajili ya kumuomba msamaha na kumbembeleza
mkewe imebuma kwa mauzo.
Albam ya ‘Paula’ inaripotiwa kuuza nakala 530 tu katika wiki yake ya
kwanza nchini Uingereza, huku Canada ikiwa imeuza nakala 550 tu katika
wiki yake ya kwanza. Marekani imeuza Units 24, 000.
Mauzo hayo yatazidi kumsononesha Robin Thicke ambaye alikuwa
akizunguka kwenye matamasha akimuomba msamaha mkewe jukwaani mara kwa
mara, huenda watu wamechoka kusikia kilio chake kuhusu mkewe.
Mauzo ya Paula ni tofauti kabisa na mauzo ya albam yake ya Blurred
Lines ambayo iliuza nakala 177,000 katika wii ya kwanza Marekani huku
ikishika nafasi ya kwaza Uingereza.
0 comments:
Post a Comment