Wiki iliyopita kuna video inayomuonesha muigizaji maarufu wa kike,
Angelina Jolie akiwa anaongea na simu kwenye chumba kichafu au tunaweza
kusema kina mazingira ya ajabu, video ambayo walipewa National Enquirer
na mfanyabiashara wa madawa ya kulevya aliyefungwa, Franlin Meyaer.
Mayer anadai kuwa alishuti kipande cha dakika 16 kwa kuruhusiwa na
Angelina Jolie mwaka 1999 katika nyumba yake ya Manhattan kumuuzia
madawa aina ya heroin na Cocaine.“Angie ni mteja wangu wa miaka mingi. Nilikuwa namuuzia heroine na
cocaine. Siku moja lainiita nyumbani kwake. Hiyo ndiyo ilikuwa njia ya
kuniambia kuwa anataka nimpelekee mzigo (dawa za kulevya). Kwa muda huo
nilikuwa nimenunua video camera na nikaamua kwenda nayo. Na nilipofika
nilimpa dawa za kulevya na yeye akanipa pesa yangu. Alionekana kutojali
nani alikuwa pale.” Ameeele Mayer.
Maelezo ya bwana Mayer yanashabihiana na maelezo ya Angelina Jolie ya
mwaka 2011 ambapo aliwahi kukaririwa akizungumzia mambo magumu
aliyowahi kuyapitia kabla hajawa mtu anaeheshimika zaidi sasa hivi na
mfano wa kuigwa kwa wanawake na jamii kwa ujumla.
“Nilipitia wakati wa mgumu, wakati wa kiza na nikavuka. Sikufa nikiwa
kijana, kwa hiyo nina bahati sana. Kuna wasanii wengine na watu abao
wahawakuweza kuvishinda vitu hivyo. Nadhani watu wanaweza kuimagine
kwamba nilifanya vitu hatari zaidi na vichafu zaidi. Kwa sababu
mbalimbali nisingeweza kuwa hapa. Unafikiria kuhusu hayo pia mara nyingi
wakati unapokuwa karibu na vitu vingi hatari, na nafasi nyingi
zimechukuliwa mbali zaidi.”Alisema Angelina Jolie
Hayo yalikuwa ya zamani, hivi sasa Angie ni muigizaji anaesaidia sana
jamii hasa wasichana wa Afrika na amejenga mashule na kutoa misaada
mbalimbali kusaidia kutokomeza udhalilishaji na unyanyasaji.
Ni mama hodari wa familia yake na muigizaji Brad Pitt.
0 comments:
Post a Comment