Wednesday, July 9, 2014

Saraha kusepa baada ya kumleta 'Shemeji'

Msanii Saraha wa nchini Sweden-Stockholm mwenye makazi yake nchini Tanzania ameelezea kuwa baada ya kuachia kibao chake kipya alichokibatiza jina 'Shemeji' hivi sasa ana mpango wa kurudi tena nchini Sweden.

                                         Msanii wa muziki nchini Saraha
Saraha ameongea na thade expensive kuwa amefurahi kuwa mashabiki wanazikubali sana kazi zake nchini na kuelezea kuwa atarudi nyumbani Sweden kwa ajili ya kuendelea kusambaza muziki wake.
Aidha, mwanadada huyo ameongezea kuwa amekwisha fanya mipango ya kufanya kazi pamoja
na wasanii nchini Sweden ambao pia wanafanya muziki wa kiafrika zaidi.
Kwa sasa dashosti huyo amerelease albam yake mpya aliyoibatiza jina 'Mbele Kiza' inayotamba Ulaya ambayo inaendelea kupata soko kubwa kupitia mitandao ya kijamii.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...