Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini amesema kuwa
viongozi wa serikali wanaohudumia maslahi yao binafsi na waasi ndio
sababu ya njaa "iliyotengenezwa na mwanadamu" nchini humo.
Hilde
Johnson anayeongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini
ameikemea serikali ya Juba la waasi kwa nafasi yao katika kuitumbukiza
hatarini zaidi Sudan Kusini ambayo amesema ni miongoni wma nchi maskini
zaidi duniani. Amesema maelfu ya watu wameuawa nchini humo na
kutahadharisha kwamba nchi hiyo sasa imerudi nyuma kwa miongo kadhaa.
Jonson amesema kuwa saratani ya ufisadi wa mabilioni ya dola
yanayotokana na mafuta imewakumba viongozi wa nchi hiyo na
kuwasababishia laana. Hilde Johnson ameyasema hayo katika maadhimisho ya
mwaka wa tatu wa kutangazwa uhuru na kujitawala Sudan Kusini.
Maelfu
ya watu wameuawa nchini Sudan Kusini na wengine zaidi ya milioni 1.3
kufukuzwa katika makazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe
kati ya jeshi la serikali na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa
rais wa Sudan Kusini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia
amezitaka pande mbili hasimu nchini humo kurejea katika meza ya
mazungumzo ya amani.
0 comments:
Post a Comment