Tuesday, September 9, 2014

Bebe Cool awa balozi wa Cranes

Mwanamuziki Moses Ssali aka Bebe Cool, amechaguliwa kuwa balozi wa timu ya taifa ya mpira wa miguu, Uganda Cranes, kwa lengo la kutumia nguvu ya ushawishi aliyonayo msanii huyu kujitangaza zaidi.

msanii Bebe Cool akiwa na wachezaji wa timu ya soka ya Uganda Cranes
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka Uganda, Moses Magogo, kwa hatua hii imani na matarajio yao makubwa ni kuona jina la timu Uganda Cranes linakwenda juu zaidi katika ngazi nyingine.
Bebe Cool mwenyewe ambaye amekuwa na mapenzi makubwa na soka, tayari amekwishaanza kuitumikia nafasi yake kwa kutangaza matukio mbalimbali kuhusiana na timu hii, hususani kupitia mitandao ya kijamii.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...