Tuesday, September 9, 2014

Mapya kuhusu hali na afya ya Michael Schumacher

Mapya kuhusu hali na afya ya Michael Schumacher

Dereva mkongwe wa mbio za magari ya Formula One, Michael Schumacher ameruhusiwa kutoka hospitali na amepelekwa Uswizi ambapo atawekwa chini ya uangalizi wa matabibu akiwa katika nyumba ya familia yake.
Afya ya Schumacher imeendelea kuimarika taratibu katika kipindi cha miezi 9 tangu apate ajali mbaya wakati akifanya mazoezi ya kuteleza kwenye milima ya barafu, December mwaka jana.
Dereva huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa katika hali mahututi kwa kipindi kirefu huku ripoti kamili kuhusu afya yake ikitolewa bila maelezo ya kina.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...