Wednesday, September 10, 2014

USA Waendeleza Mikakati Ya Kutetea Ubingwa Wa Dunia

USA Waendeleza Mikakati Ya Kutetea Ubingwa Wa Dunia

Hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia ya mpira wa kikapu imeshuhudia timu mbili zikitangulia kwenye hatua ya inayofuata usiku wa kuamkia hii leo baada ya kufanikiwa kupata ushindi dhidi ya timu pinzani.
Mabingwa watetezi wa fainali hizo timu ya taifa ya Marekani waliwafunga midomo Slovenia baada ya kuwachapa point 119 – 76.
Mchezo mwingine wa hatua ya robo fainali uliochezwa jana huko nchini Hispania ulishuhudia Lithuania wakiwaangamiza Uturuki waliokubali kibano cha point 73–61.
Hii leo michezo ya hatua ya robo fainali itahitimishwa kwa timu nyingine mbili zitakazokwenda kwenye hatua ya nusu fainali ambapo;
Serbia                   vs.                Brazil
Waamuzi: Steven Anderson (USA), José Reyes (MEX), Borys Ryzhyk (UKR)

Ufaransa              vs.                Spain
Waamuzi: Luigi Lamonica (ITA), Michael Aylen (AUS), Oļegs Latiševs (LAT)

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...