Mhudumu wa bar kutoka Ujerumani ameweka rekodi ya dunia kwa kubeba
glasses 27 za bia kwa mkupuo kwa mikono miwili aliyojaliwa na Mungu.
Mhudumu huyo aliyetajwa kwa jina la Oliver Struempfel alibeba glasses
hizo zilizojaa bia na kuzifanya kuwa na uzito wa Kilogram 62 kisha
akatembea nazo umbali wa mita 40 bila kudondondosha wala kumwaga tone.
Struempfel aliweka rekodi hiyo katika shindano maalum la tamasha la
beer huko Abensberg linalojulikana kama ‘Gillamoos beer Festival’ baada
ya kumshinda mpinzani wake ambaye aliweza kubeba glasses 26.
Nimefanya kazi hapa kwenye biashara ya beer (kama mhudumu) tangu
miaka 17 iliyopita, kwa hiyo nina mafunzo mengi.” Amesema Struempfel.
0 comments:
Post a Comment