BAADA ya
saluni yake iliyopo Sinza jijini Dar kufungwa huku uvumi wa kudaiwa
kufulia ukimuandama, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka
kuwa uvumi huo hauna ukweli.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Nisha alisema biashara yake ya saluni ipo kama
kawaida ila ameihamishia maeneo ya Chuo Kikuu - Mlimani kwa kuwa eneo la
awali halikuwa na nafasi kubwa.
“Sijafulia
hata kidogo hayo ni maneno tu yanayozagaa, saluni yangu nimeihamishia
Mlimani jamani, nashangaa kweli kwa wanaosema nimefulia,” alisema Nisha.
0 comments:
Post a Comment