Thursday, October 23, 2014

Tanzania imejizatiti kukabiliana na Ebola

Baada ya kukanusha uvumi kuhusu uwepo kwa ugonjwa wa Ebola, serikali ya Tanzania imesisitiza kwamba ina uwezo pamoja na vifaa vya kutosha vya kukabiliana na ugonjwa Ebola iwapo kutatokea mlipuko wa ugonjwa huo hapa nchini.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe Steven Kabwe, amesema hayo jana , juu ya jitihada za serikali katika kuhakikisha kuwa virusi vya ugonjwa huo haviingii nchini.
Kwa mujibu wa Dkt Kebwe, hivi sasa kuna vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupima watu wote wanaowasili nchini kupitia katika mipaka na viwanja vya ndege, na kwamba idadi kubwa ya wahudumu wa afya wamepata mafunzo ya namna ya kutambua, kudhibiti kusambaa pamoja na kuhudumia mtu atakayebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola.
Hata hivyo, waziri Kebwe amesema kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika nchi za Afrika Magharini hakuwezi kuifanya Tanzania ibweteke na kulegeza hatua inazochukua sasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...