Thamani ya soko la biashara ya rejareja kupitia mtandao wa Internet
nchini China ilifikia dola bilioni 296 za kimarekani kwa mwaka jana, na
kuifanya China kuongoza katika soko hilo duniani.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya
China, biashara hiyo iliendelea kuongezeka kwa kasi kwa asilimia 32.5
kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana wakati
kama huo.
Wakati huohuo China inaendelea kutunga sheria kuhusu biashara ya
mtandao wa Internet ili kuondoa matatizo yaliyopo sasa kama vile
utapeli, bidhaa feki na kutumiwa vibaya kwa taarifa binafsi za wateja.
0 comments:
Post a Comment