Tuesday, June 24, 2014

roma:nimefanya kazi nyingi na wasani wengine siwabagui wasanii wenzangu

Kufuatia rapa ROMA kuonekana kama msanii asiyekuwa na utamaduni wa kufanyakazi ama kolabo na wasanii wenye majina makubwa nchini, kutokana na kuwa na rekodi chache ambazo amefanya na mastaa wenzake, amefunguka na kuwatoa hofu mashabiki wake.
Rapa Roma akishika tuzo zake
Rapa huyu ameweka wazi kuwa kuna kazi nyingi ambazo amefanya na wakali wenzake ambazo zipo hazijatoka.
Kama ulikuwa ufahamu, ROMA amewataja wasanii wakubwa ambao amekwishafanya nao kazi akiwepo MwanaFA, Mwasiti na wengine huku akiweka wazi kuwa kwa sasa yupo katika mpango wa kufanya 'duet' na msanii Chidi Benz, mpango ambao ulikuwa katika ratiba kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment