Sunday, November 24, 2013

update:baada ya makubaliano iran

Baada ya kufikiwa makubaliano kati ya Iran na kundi la 5+1, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kuwa makubaliano hayo ni hatua ya kwanza na kwamba pande mbili zinapaswa kuendelea kushirikiana kwa msingi wa kuheshimiana pande mbili na maslahi ya pamoja. Akizungumza mwishoni mwa mazungumzo hayo mjini Geneva Muhammad Javad Zarif ameishukuru serikali ya Uswisi kwa kuwa mwenyeji mzuri wa mazungumzo hayo, Umoja wa Mataifa na pia Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya.
Vikwazo vya Iran kuanza kupunguzwa wiki zijazoWaziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, vikwazo vitaanza kupunguzwa baada ya wiki mbili au tatu zijazo na kusisitiza kuwa, vituo vya urutubishaji havitofungwa na kwamba shughuli za maji mazito zitaendelea kama kawaida.
 Leo alfajiri, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefikia mapatano ya nyuklia na nchi sita zenye nguvu duniani baada ya mazungumzo magumu yaliyoendelea kwa muda wa siku nne mfululizo mjini Geneva Uswisi. Nukta muhimu katika mapatano hayo ni kutambuliwa haki ya Iran ya kurutubisha madini ya urani inayotumika kuzalisha nishati ya nyuklia. Aidha shughuli za nyuklia za Iran zitaendelea sambamba na kupunguzwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...