Rapper Kanye West ameamriwa na mahakama ya Los Angeles kufanya kazi
za jamii kwa kipindi cha masaa 240 na kuwa chini ya kipindi cha
matazamio ‘probation’ kwa miaka miwili kutokana na tukio la kumshambulia
mpiga picha.
Kesi hiyo ilifunguliwa kutokana na tukio alilofanya mwezi July mwaka
jana ambapo alimshambulia mpiga picha aliyejaribu kumpiga picha katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, ilielezwa kuwa kutokana na uchunguzi
imeonekana kuwa July 19, 2013 mpiga picha anaejulikana kama Daniel
alikuwa amesimama katika uwanja huo wa ndege akimsubiri Kanye West, na
alipomkaribia alimuuliza kama anaweza kuongea nae.
Daniel alipoona Kanye yuko kimya akauliza swali lingine, ‘Kwa nini
hatuwezi kuongea na wewe?’ Swali ambalo lilitokana na kauli ya Kanye
West wiki kadhaa zilizopita kuwa hataki paparazzi amuengeleshe wala mtu
yeyote.
Imeelezwa kuwa Kanye West aliweka begi chini akamfuata Daniel kama
anataka kuongea nae vizuri na kisha bila kughafirishwa na neno lolote
toka kwa Daniel alimvamia na kumshambulia huku akijaribu kumnyang’anya
kamera yake.
Kutokana na purukushani hizo Daniel alianguka chini huku akiwa
ameishikilia kamera yake na kuumia magoti na ‘hip’ na kupata maumivu
makali. Alipelekwa hospitalini na Ambulance ambako aliwekwa katika
chumba cha dharura.
Mahakama pia imemhukumu Kanye West kuhudhuria vipindi 24 vya daraja la pili la program ya kudhibiti hasira.
Hata hivyo Kanye West hakuwa mahakamani hapo na hivyo anatakiwa
kuripoti polisi jijini Los Angeles. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa
tena July 17 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment