Baada ya kuachia ngoma ya Mfalme ambayo mitaa imeielewa kwa kiasi
kikubwa, Mwana FA ameweka wazi kuwa, wazo la kusuka ngoma hii ni kuweka
wazi mambo yanayoizunguka jamii, kuikumbusha kuwa kadri kila mtu
anavyojiona kuwa hana, kuna ambao hawana zaidi.
Mwana
FA pia amefunguka kuwa, kutokana na kupenda kufanya muziki mzuri,
anafeel sana muziki wa G Nako na pia alikuwa na mipango ya siku nyingi
ya kufanya kazi na Nahreel ili kutengeneza muunganiko ambao watu
watauelewa zaidi.
Kuhusiana na mipango ya video ya kazi hii, Mwana FA akatuchana kuwa mipango imeshapangika, na ndani ya wiki hizi mbili watasafiri kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya kufanya kazi hii ambayo amepewa Director Kelvin Bosco Jr.

No comments:
Post a Comment