Sunday, May 18, 2014

Jay Z anakanyaga nyayo za uhusiano wa mapenzi ya Damon Dash kutoka kwa Aaliyah hadi kwa Rachel Roy?

Jay Z anakanyaga nyayo za uhusiano wa mapenzi ya Damon Dash kutoka kwa Aaliyah hadi kwa Rachel Roy?
Ugomvi wa Jay Z na Solange umezua mengi licha ya wanafamilia hao kutoa tamko rasmi na kuiambia dunia kuwa wameyamaliza.
Uamuzi wa Solange kumpiga vibao nguli wa rap duniani, Jay Z ndio kichocheo cha watu kutakaka kufahamu nini hasa mzizi wa ugomvi huo hata kama wao wameyamaliza.
Chanzo kiliieleza E! kuwa ugomvi huo ulichochewa zaidi na designer Rachel Roy ambaye alijiweka karibu sana na Jay Z hali ambayo ilimuudhi Beyonce ambaye alishindwa kuvumilia na kumpa makavu huku Solange akimuunga mkono na kumpa onyo.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa majibu ya Jay Z ndiyo yaliyochochea ugomvi zaidi ambapo yeye aliichukulia poa vitendo vya Rachel Roy hali iliyowafanya ndugu hao (Beyonce na Solange) kuhisi na yeye anataka iwe anavyotaka Rachel Roy.
Hii inachukuliwa kama sababu ya Beyonce kumuunga mkono Solange kumpa vibao Jay Z aliyetaka kwenda kwa Rihanna bila yeye huku Rachel Roy pia akielekea huko.
Ikumbukwe kuwar Rachel Roy aliwahi kuwa mke wa Damon Dash ambaye pia aliwahi kumchumbia marehemu  Aaliyah.
Sasa Jay Z ameonesha kuwa interested na Rachel Roy na inaripotiwa kuwa Jay Z pia aliwahi kuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Aaliyah!
Hali hii ndiyo imezua swali ama kuonesha hali ya Jay Z kuzifuata nyayo za uhusiano wa mapenzi wa Damon Dash kwa Rachel Roy na Aaliyah.
Hii iliwekewa alama zaidi baada ya Beyonce kupost kwenye instagram picha akiwa amevaa Sweta lenye picha ya Aaliyah siku moja baada ya ugomvi wa Solange na Jay Z.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...