
Ugomvi wa Jay Z na Solange umezua mengi licha ya wanafamilia hao kutoa tamko rasmi na kuiambia dunia kuwa wameyamaliza.
Uamuzi wa Solange kumpiga vibao nguli wa rap duniani, Jay Z ndio
kichocheo cha watu kutakaka kufahamu nini hasa mzizi wa ugomvi huo hata
kama wao wameyamaliza.
Chanzo kiliieleza E! kuwa ugomvi huo ulichochewa zaidi na designer
Rachel Roy ambaye alijiweka karibu sana na Jay Z hali ambayo ilimuudhi
Beyonce ambaye alishindwa kuvumilia na kumpa makavu huku Solange
akimuunga mkono na kumpa onyo.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa majibu ya Jay Z ndiyo yaliyochochea ugomvi
zaidi ambapo yeye aliichukulia poa vitendo vya Rachel Roy hali
iliyowafanya ndugu hao (Beyonce na Solange) kuhisi na yeye anataka iwe
anavyotaka Rachel Roy.
Hii inachukuliwa kama sababu ya Beyonce kumuunga mkono Solange kumpa
vibao Jay Z aliyetaka kwenda kwa Rihanna bila yeye huku Rachel Roy pia
akielekea huko.
Ikumbukwe kuwar Rachel Roy aliwahi kuwa mke wa Damon Dash ambaye pia aliwahi kumchumbia marehemu Aaliyah.
Sasa Jay Z ameonesha kuwa interested na Rachel Roy na inaripotiwa
kuwa Jay Z pia aliwahi kuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Aaliyah!
Hali hii ndiyo imezua swali ama kuonesha hali ya Jay Z kuzifuata
nyayo za uhusiano wa mapenzi wa Damon Dash kwa Rachel Roy na Aaliyah.
Hii iliwekewa alama zaidi baada ya Beyonce kupost kwenye instagram
picha akiwa amevaa Sweta lenye picha ya Aaliyah siku moja baada ya
ugomvi wa Solange na Jay Z.






Dar+Es+Salaam
0 comments:
Post a Comment