Friday, May 16, 2014

Mabomu mawili yaua watu 10 Nairobi

nairobiMilipuko miwili imetokea kwenye eneo la soko la Gikomba katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na kuua watu wasiopungua 10 na kujeruhi wengine wengi, wamesema maafisa.
Chanzo za milipuko hiyo hakijajulikana ila Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mabomu miaka ya karibuni.
Wamekuwa wakililaumu kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab kutoka nchi ya jirani ya Somalia.
Mamia ya watalii wa Uingereza wameondolewa kutoka kwenye maeneo ya pwani ya Mombasa kufuatia onyo la shambulizi.
Makampuni ya utalii ya Uingereza yamesitisha safari za Mombasa, mji mkubwa wa pili Kenya.
Kituo cha uokoaji wa Maafa cha Kenya kimedai kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea kwenye basi dogo, la pili kwenye soko kubwa la wazi la Gikomba.
Mabomu hayo yamelipuka ikiwa ni siku mbili baada ya Uingereza, Ufaransa na Marekani kuonya kuwa kuna hatari ya mashambulizi nchini Kenya.
Kenya walipinga mataifa hayo kwa kutoa maonyo yao.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...