Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limezima maandamano ya wafanyakazi wa
Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), huku abiria zaidi ya 200
wakirudishiwa nauli zao kutokana na mgomo ulioanza tangu Mei 12 mwaka
huu.
Wakizungumza
na wafanyakazi Mwenyekiti wa kanda wa chama cha Wafanyakazi wa Reli
nchini (TRAWU) Bw. Yusuph Mandai na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya
wanawake (TUCTA) Bi. Rose Mwambe wamesema kuwa hawapo katika mgomo ila
wanashinikiza uongozi kuwasikiliza na kuwalipa mshahara, na kudai kuwa
mpaka Serikali itakapowalipa mishahara yao ya Februari hadi Mei ndipo watakapoendelea na kazi.
Naye mmoja wa wafanyakazi hao ameeleza kuwa wao ni watoa huduma kama wengine na hawawezi kufanya kazi kama hamna chakula na kuongeza kuwa kutolipwa kwao mshahara kumewaathiri kiuchumi.
Mgomo huo umesababisha kuahirishwa kwa safari za Dar es Salaam kwenda Kapirimposhi Zambia na Dar es Salaam na Mwakanga mpaka madai yao yatakaposikilizwa.
Wakizungumza na East Africa Radio abiria Joyce Godfrey na Hasani Mwera wamesema walitegemea kusafiri kesho lakini wamefika hapo na kuelezwa kuwa huduma ya usafiri imesitishwa kutokana na mgomo wa wafanyakazi.

No comments:
Post a Comment