
Wakati bado dunia imeshindwa kufahamu mahali ilipo ndege ya Malaysia
(Flight MH370) iliyopotea huku ndugu na jamaa wakiwa na majonzi ya
kutojua hatma ya wapendwa wao, mtayarishaji Rupesh Paul yeye ameamua
kutayarisha filamu inayohusu tukio hilo.
Rupesh Paul ambaye ni raia wa India tayari ameanza kutayarisha filamu
hiyo huku watu wakiwa hawafahamu hata nini chanzo hasa cha kupotea kwa
ndege hiyo na matukio yaliyojiri ndani ya ndege.
Mtayarishaji ameiambia Hollywood Reporter kuwa filamu hiyo haitaumiza
hisia za ndugu na jamaa za abiria waliopotea na ndege hiyo na kwamba
hakuna matumizi yoyote ya bunduki yatakayooneshwa.
“Haitahusu vitu vya kijinga. Hakutakuwa na matumizi ya bunduki na
hakutakuwa na matumizi mabaya ya vitu vya kigeni.” Alisema Rupesh Paul.
Katika kutetea uamuzi wake wa kutumia tukio hilo kama sehemu ya
filamu yake, alieleza kuwa haoni umuhimu wa kutengeneza filamu ambayo
haiwavutii watu.
“Watu hawataki Makala, wanataka kitu kitakachowasisimua. Kwa nini
nitayarishe filamu kuhusu kitu kingine chochote ambacho hakiwavutii
watu?” Alihoji.






Dar+Es+Salaam
0 comments:
Post a Comment