Friday, June 27, 2014

Madtraxx amtupia dongo Vera

Mtayarishaji, Msanii wa muziki na pia DJ, Madtraxx kupitia mtandao ametoa ujumbe ambao unahisiwa kuelekezwa kwa mwanadada Vera Sidika, kwa ajili ya kuponda hatua yake ya kuingia gharama na kubadili rangi halisi ya ngozi yake ili kuwa mweupe.

                              Msanii wa Kenya Vera Sidika
Madtraxx, kufuatia taarifa za Vera kugharamia kubadili ngozi yake kwa kitita cha shilingi za Kenya milioni 50, ameweka picha yake akiwa na mrembo mwenye rangi nyeupe asilia, sambamba na maneno kuwa hajalazimika kugharamia milioni 50 kumpatia mrembo huyu muonekano alionao.
Kitendo cha mwanadada Vera kuingia gharama kuongeza weupe katika ngozi yake kimepokelewa tofauti na watu mbalimbali, huku wengi wakifikiri kuwa si mfano mzuri kujiondoa katika uhalisia kwa ajili ya kusaka urembo.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...