Sunday, June 22, 2014

Octopizzo apozi na wakimbizi

Rapa Octopizzo ameonyesha moyo wake wa upendo kwa kutumia muda wa kutosha kushiriki katika shughuli za msaada pamoja na kukaa na wakimbizi katika kambi ya Kakuma iliyopo huko nchini Kenya.

              Rapa Octopizzo akipozi na wakimbizi Kakuma Kenya
Octopizzo kufuatia tukio hili amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, kuhudumia wengine ndiyo thamani ama kodi ya maisha ya kila mmoja hapa duniani.
Msanii huyu amesema kuwa, anapenda maisha yake yatafsiriwe kwa kile ambacho anakiandika katika mioyo ya watu aliowagusa, na si kwa kile kitakachoandikwa katika kaburi lake pale utakapofika mwisho wa maisha yake.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...