Dr Dre na Jimmy Lovin ambao wanaendelea kushangilia kuwa mabilionea
baada ya kuwauzia Apple kampuni yao ya Beatz Electronics kwa $ Billion 3
tu, wamepata mshituko baada ya kugundua kuwa Makampuni ya kichina
yameingiza pesa hiyo zaidi ya mara 40 kwa kuuuza headphones fake za
‘Beatz By Dre’.
Kwa mujibu wa TMZ, makampuni mengi ya China yamegundulika kuwa
yalikuwa yanatengeneza headphones zenye logo ya Beats na kuuza kwa bei
nafuu dunia nzima kwa njia ya mtandao wakitumia tovuti mbalimbali.
Dr Dre amekasirishwa na hatua hiyo na amefungua mashtaka dhidi ya
makampuni hayo na kitu cha kwanza alichoiomba mahakama ni kuhakikisha
kwanza wanachukua majina ya ‘domain’ za tovuti zote zinazofanya biashara
hiyo na pia kuhakikisha faida zote zinazopatikana kwenye mauzo hayo.
0 comments:
Post a Comment