Mabingwa wa zamani wa soka mkoa wa Kilimanjaro, Machava FC ya mjini Moshi imedunguliwa mabao 2-0 na mahasimu wao Kitayosce FC ya mjini humo katika mchezo wa kirafiki.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa King George Memorial mjini Moshi Kitayosce walianza kuliona lango la Machava FC katika dakika ya 10 ya mchezo Haruna Juma akifumania nyavu baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Hemed Rashid upande wa kushoto wa uwanja.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Kitayosce kuongoza, ambapo katika dakika ya 60 ya mchezo Carol Anthony “Chimco” akiwa na Stanley walimchezea rafu mchezaji wa Machava na mwamuzi kuipa penati ambayo walikosa.
Chimco aliweza kufumania nyavu kunako dakika 69 ya mchezo lakini bao lake lilikataliwa na mwamuzi.
Katika dakika ya 80 ya mchezo alikuwa Kibwana Abdallah akitokea benchi aliipatia bao Kitayosce akimalizia mpira wa adhabu kwa kichwa uliopigwa na Meshacollins na kuguswa na Chimco, hivyo matokeo kusomeka 2-0.
Timu zote mbili zinajiandaa kwa Ligi itakayoanza kutimua vumbi mwezi Agosti mwaka huu, Kitayosce FC itakuwa Ligi ya Wilaya ya Moshi na Mabingwa hao wa 2012/2013 watakuwa na Ligi ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Kitayosce FC: Coach Hamad Haule
Machava FC: Coach Hamad Mwaliko
0 comments:
Post a Comment