Msanii wa muziki wa kike wa miondoko ya Afro Pop nchini Vanessa Mdee
aliyetwaa tuzo ya Kili Music kwa mwaka huu kwa wimbo wake 'Hawajui' yupo
mbioni kufanya kolabo na kundi la Sauti Sol nchini Kenya.
Vanessa
Mdee ambaye hivi karibuni amefanya kolabo na wasanii wa kike nyota wa
Kenya wakiwemo Victoria Kimani na Xtatic, ameelezea kuwa anajiandaa
kuingia studio na kundi hilo litakaporudi likitokea nchini Amsterdam
katika ziara ya muziki.
Hivi sasa dashosti huyo anafanya vyema na kichupa chake kipya cha wimbo wake 'Come Over' kilichotayarishwa na prodyuza Nahreel.
Hivi sasa dashosti huyo anafanya vyema na kichupa chake kipya cha wimbo wake 'Come Over' kilichotayarishwa na prodyuza Nahreel.

0 comments:
Post a Comment