Usiku wa jana mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Fernando Torres
alikamilisha usajili wake wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea kwenda
AC Milan.
Huku yakiwa hajapita hata masaa 24 tangu Torres aondoke, Jose
Mourinho amekamilisha usajili wa mbadala wa Torres, mshambuliaji wa
kimataifa wa Ufaransa Loic Remy.
Remy ambaye alifeli vipimo vya afya alipokuwa akikaribia kujiunga na
Liverpool mwanzoni mwa dirisha la usajili, amejiunga na Chelsea kwa ada
ya uhamisho wa paundi millioni 10 kutoka QPR.
Remy anachukua nafasi ya Torres na kuungana na Didier Drogba katika kumsaidia Diego Costa.
Wakati huo huo Alex Song amejiunga na West Ham kwa mkopo kutoka FC Barcelona.
0 comments:
Post a Comment