Akikonga nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja wa Lake Tanganyika
kupitia Tamasha kubwa la Kili Music Tour mkoani Kigoma, Christian Bella
amejipanga kuonyesha heshima kubwa kwa akina mama jijini Dar es Salaam.
Christian
Bella aka Mzee wa Masauti ameongea na enewz kuwa ameandaa tukio hilo
kubwa la Live lililobatizwa jina 'Usiku wa Nani Kama Mama
litakalofanyika tarehe 29 mwezi huu, lengo kubwa la show hiyo ni ya
kutoa heshima kubwa kwa akina mama ambao ndio watu muhimu katika jamii
duniani.
Mfalme huyo wa masauti ameelezea kuwa show hiyo itakuwa ni Live ambapo mkali huyo amewashirikisha wasanii maarufu watakaomsindikiza stejini akiwemo Ommy Dimpoz aliyeshirikishwa katika wimbo huo, wengine watakaompa tafu live stejini ni wasanii Banana Zorro, Matonya, Cassim Mganga, Dully Sykes pamoja na bendi ya Malaika.

0 comments:
Post a Comment