Mtoto wa Jackie Chan ambaye pia ni muigizaji wa filamu za mapigano,
Jaycee Chan anaendelea kushikiliwa na polisi nchini China kwa kosa la
kukutwa na dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa polisi wa Beijing, Jaycee alikamatwa akiwa na muigizaji
mwenzake wa Taiwan, Kai Ko na kwamba baada ya kupimwa waligundulika
kuwa walikuwa wametumia dawa za kulevya aina ya marijuana.
Jaycee na Kai Ko wamekiri kutumia dawa hizo na kueleza kuwa grams 100
za dawa hizo zilipelekwa nyumbani kwa Jaycee (mtoto wa Jackie Chan).
Baada ya kushikiliwa kwa wiki mbili (tangu August 14), Kai Ko
ameachiwa Ijumaa iliyopita na anasubiri taratibu zaidi za kisheria huku
Jaycee akiendelea kusota rumande.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Beijing, waandishi wa habari
walimfuata Kai Ko hadi kwenye hotel aliyofikia lakini hakuonesha
ushirikiano na alijaribu kumpiga mwandishi mmoja kabla hajaingia kwenye
lift na kutokomea.
Baada ya kukamatwa na dawa hizo, Jackie Chan aliomba radhi umma kwa
niaba ya mwanae na familia yao kwa ujumla alimtaka mwanae kuelewa kuwa
amefanya makosa na anapaswa kukutana na matokeo yake.
0 comments:
Post a Comment