Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema jeshi hilo
linamshikilia mtuhumiwa wa matukio ya kuwapiga risasi wanawake jijini
Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo , Kamanda Liberatus Sabas amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 26 mwaka huu, majira ya usiku, nyumbani kwake Majengo Juu.
Kamanda Sabas amesema baada ya kumkamata mtuhumiwa na kumhoji ambapo alikiri kuhusika katika matukio yanayoendelea jijini Arusha ya upigaji wanawake risasi na moja kati ya silaha hizo iliibiwa ndani ya gari la mfanyabiashara Seleman Bakari Msuya mkazi wa Sombetini, baada ya watu wasiojulikana kuvunja kioo cha gari na kuichukua. Mtuhumiwa anatarakiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kumalizika.
Kamanda Sabas ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa siri za mtandao huo uliozuka ghafla mwezo Agosti mwaka huu na kujeruhi na kuua wanawake wenye magari mjini Arusha, ambapo hadi sasa tayari watu nane wanashikiliwa kwa kuhusiana na matukio hayo.
0 comments:
Post a Comment