Rapa Stereo ambaye ameachia kwa mashabiki wake kolabo yake ya Kimataifa,
"Wako", featuring Victoria Kimani, ameweka wazi sababu za kazi hii
kuchelewa kuachiwa, ambapo amesema kuwa ni kutokana na Video ya Usione
Hatari kuchelewa kutoka.
Stereo
amesema kuwa, aliamua kutoa muda kwa kazi yake hii iliyotangulia,
Usione Hatari kuwakaa mashabiki wake kabla ya kuwahamishia katika jiwe
jingine, Wako ambalo tayari limepokelewa vizuri mitaani na mashabiki wa
muziki.
Kuhusiana na video ya kazi hii mpya ya kimataifa, Stereo amesema kuwa baada ya wiki mbili tatu, atakuwa ameweka mambo kwenye mstari.
Kuhusiana na video ya kazi hii mpya ya kimataifa, Stereo amesema kuwa baada ya wiki mbili tatu, atakuwa ameweka mambo kwenye mstari.
0 comments:
Post a Comment