Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari kuhusu uwepo wa
mwanamieleka mkongwe, Hulk Hogan katika jiji la Lagos. Ingawa kwa
muonekano anaonekana ndiye lakini inaelezwa kuwa mtu huyo sio Hulk Hogan
halisi.
Mtu huyo ameonekana akizunguka mitaa akiwa juu ya gari huku umati wa
mashabiki ukimfuata na amepewa ulinzi mkali wa polisi ambao ni vigumu
kuamini kuwa ni kweli atakuwa fake.
Mitandao ya Nigeria imeeleza kuwa, Hulk Hogan halisi hajafika Nigeria
na kwamba inawezekana kabisa kuna mtu amefanya mchongo huo ili kuwaibia
watu.
Taarifa za Hulk Hogan Fake zimefananishwa na zile za PSY wa Gangnam
Style aliyewahi kuingia nchini humo na kupewa mapokezi na matunzo ya
daraja la kwanza kabla hajajulikana kuwa sio PSY halisi.
Kilichomuumbua PSY huyo ambaye ilikuwa vigumu kumtofautisha, ni pale PSY halisi alipoonekana akiga show Marekani siku hiyo hiyo.
Hapo hali ilibadilika Lagos kwa PSY aliyekuwepo na alikamatwa na vyombo vya usalama.
PSY halisi(kushoto), PSY fake (Kulia/mwenye koti jeusi)
0 comments:
Post a Comment