Mabingwa wa soka duniani timu ya taifa ya Ujerumani
wamefanikiwa kuwasambaratisha Scotland katika mchezo wa kusaka nafasi ya
kufuzu kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 ambazo
zitafanyika nchini Ufaransa.
Ujerumani ambao walikuwa na uchungu wa kupoteza mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Argentina kati kati ya juma lililopita, walifanikisha azma ya ushindi katika mchezo wa kundi lao dhidi ya Scotland kwa kuwabanjua mabao mawili kwa moja.
Mabao hayo ya mabingwa wa dunia yalifungwa na mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Thomas Mueller katika dakika ya 18 na 70 huku Ikechi Anya akifunga bao la kuwafuta machozi waskotish waliokuwa wanaufuatialia mchezo huo.
Michezo mingine ya kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo ni kati ya;
Georgia 1 - 2 Jamuhuri ya Ireland
Hungary 1 - 2 Ireland ya kaskazini
Gibraltar 0 - 7 Poland
Visiwa vya Faroe 1 - 3 Finland
Greece 0 - 1 Romania
Denmark 2 - 1 Armenia
Ureno 0 - 1 Albania

0 comments:
Post a Comment