Barnaba ambaye ameutaja mwaka huu kuwa mwaka wake wa mafanikio zaidi
ameelezea mpango wa safari yake kwenda Ufaransa na Marekani mwezi huu.
msanii huyo amesema
kuwa safari yake italenga katika kukamilisha collabo yake na Fally Ipupa
pamoja na video lakini pia ataenda New York kwa ajili ya mradi wa
Malaria No More.
“Panapomajaliwa katikati ya mwezi ujao naenda Ufaransa. Nikitoka
Ufaransa narudi tena New York na baada ya hapo narudi Dar. Kwa ajili ya
Hawalade lakini pia kwa ajili ya project nyingine. Kwa sababu mimi pia
ni balozi wa malaria no more, kwa hiyo naenda kama balozi ambaye naenda
kuchukua elimu kidogo.”
“Lakini Ufaransa naenda kwa ajili ya Fally Ipupa. Naenda kufanya
collabo nae na wimbo wangu pia nafanya nae. Huo wimbo ulifanyika ulikuwa
nusu hakumaliza. Kwa hiyo inabidi nimfate kule tumalizie kule. Masters
nitafanyika kule na video ntafanyia kule panapo majaliwa.”
0 comments:
Post a Comment