Wednesday, March 18, 2015

Kupendeza muhimu kuelimika muhimu zaidi-Wema

Bi dada Wema Sepetu ambae ni mwigizaji katika tasnia ya Bongo Movie amefunguka na kuweka wazi kuwa urembo au kupendeza tu haitoshi katika maisha ya binadamu bali jambo kubwa na la msingi katika maisha ni kupendeza na pia kuongeza maarifa katika
                                             Wema Sepetu akipata maarifa.
nyanja mbalimbali ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupambana na vikwazo pindi unapokutana nayo,Wema Sepetu amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Inst gram.
Wema Sepetu amewataka watanzania kujifunza na kuongeza maarifa mbalimbali kwani elimu haina mwisho hivyo si vibaya kama watajitolea muda wao kuongeza maarifa kwani yeye anakili wazi kuwa anajifunza vingi katika maisha ya kila siku,maana kupendeza tu haisaidii kama hutakuwa na elimu ya mambo mbalimbali.
"Kupendeza ni muhimu ila kuelimika ni muhimu zaidi.Je, unajaribu kujifunza kitu kipya kila siku? Elimu haina mwisho na Mimi binafsi najifunza mengi kwa kaka angu Mr problem solved.Jitahidi kujiendeleza kimawazo na hautakwama ukikutana na vikwazo"
Mbali na hilo pia Diva huyo wa bongo Movies ameonyesha kuwa ni #ZamuYako2015 kufanya jambo ambalo litabadili maisha yako na kuweka historia nyingine katika maisha yako kwa kuthubutu na kufanya mabadiliko chanya yenye lengo la kuinuana kama vijana.
"Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu,tushashabikia vya kutosha.Imefika hatua ya kunyanyuana,sio kushushana.Kuelimishana,sio kusemana.Kupeana moyo,sio kukatishana tamaa."
"Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!"Aliongeza Wema Sepetu.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...