Mwanamme mmoja wa umri wa makamu, anatibiwa katika hospitali moja nchini
Pakistan baada ya kuchomwa kwa tindi kali iliyomsababishia majeraha ya
asilimia hamsini.
Mwanamke anayelaumiwa kummwagia tindi kali hiyo amekamatwa.
Familia ya mwanamme huyo, inasema mwanamke alikasirika baada ya mwanamme huyo kukataa kumuoa licha ya wao kuwa na uhusiano.
Mashambulizi ya kutumia tindi kali ni mengi dhidi ya wanawake nchini Pakistan lakini sio rahisi kuendeshwa dhidi ya wanaume.
0 comments:
Post a Comment