Mtayarishaji, Msanii wa muziki na pia DJ, Madtraxx kupitia mtandao
ametoa ujumbe ambao unahisiwa kuelekezwa kwa mwanadada Vera Sidika, kwa
ajili ya kuponda hatua yake ya kuingia gharama na kubadili rangi halisi
ya ngozi yake ili kuwa mweupe.
Msanii wa Kenya Vera Sidika
Madtraxx,
kufuatia taarifa za Vera kugharamia kubadili ngozi yake kwa kitita cha
shilingi za Kenya milioni 50, ameweka picha yake akiwa na mrembo mwenye
rangi nyeupe asilia, sambamba na maneno kuwa hajalazimika kugharamia
milioni 50 kumpatia mrembo huyu muonekano alionao.
Kitendo cha mwanadada Vera kuingia gharama kuongeza weupe katika ngozi yake kimepokelewa tofauti na watu mbalimbali, huku wengi wakifikiri kuwa si mfano mzuri kujiondoa katika uhalisia kwa ajili ya kusaka urembo.

0 comments:
Post a Comment