Mwanamuziki wa pop wa Nigeria Adokiye ambaye pia ni balozi wa Umoja wa
Mataifa ameibua mitazamo tofauti kwenye mitandao ya jamii baada ya
kusema yupo tayari kujitoa yeye kwa Boko Haram ili waachiwe wanafunzi
wasichana 276 iliyowateka.
Adokiye
ambaye ni msichana wa umri wa miaka 23, ametoa pendekezo hilo kwa
jarida moja la Nigeria, ambapo kama hiyo haitoshi amesema yupo tayari
kupoteza ubikira wake kama sharti la kuachiwa wanafunzi hao.
Mwanamuziki huyo ambaye pia ni muigizaji anayetokea jimbo la Imo, amesema amekuwa akiwawaza wasichana hao wadogo ambao wengine ni wenye umri wa kati ya miaka 11 na 12 na kushindwa kujua nini kinawatokea huko walipo.

0 comments:
Post a Comment