Aliyekua mkali wa hip hop nchini, Chid Benz AKA Chuma ameamua kurejea upya kwenye game baada ya kupotezwa kwa muda muda mrefu.
Chid anatarajia kuachia ngoma inayoitwa CHUMA aliyoifanya na Ray Vanny wa WCB na beat ikiwa imegongwa na maproducer wawili Laizer pamoja na Mr. T'touch.
Hii ni ngoma ya kwanza Chid Benz, ambae kwa sasa yuko chini ya Babu Tale baada ya kutoka Rehab Bagamoyo. Alipopelekwa kutokana na kuonekana kwenye mitandao kuwa kaharibiwa sana na dawa za kulevya.
0 comments:
Post a Comment