Producer na msanii kutoka Sharobaro records, Bob Junior anaingia kwenye vichwa vya habari baada ya skendo kuwa ana mahusiano na mke wa mtu kisha kumpost Instagram huku akiuliza "je ni yupi" akimaanisha kati ya wanaozungumziwa ni yupi kati yao ndo mwenyewe.....
Aidha wadau mbalimbali walioipata skendo hiyo wamemchana bob J kuwa afanyalo sioo issue kabisa...
Stori Kamili
Akilalamika katika kipindi cha Leo Tena, mme wa binti huyo ameeleza kuwa "yeye na huyo binti wana'ndoa halali, tena wamejaliwa kupata watoto wawili mmoja ni mdogo kabisa"
Aidha mme ameeleza kuwa, mkewe alipotea nyumbani na kuitelekeza familia, jambo lililopelekea kaka wa binti huyo kumtafta na kumuadabisha. Tabia hiyo haikukoma binti huyo alitoweka nyumbani na kuibukia kwa Bob junior.
Jamaa anadai kuwa marafik zake walianza kuona picha za mkewe zikipostiwa na Junior kama video queen wa video mpya ya Sharobaro. Jambo hilo limepelekea jamaa kuhakiki na kutaka kupeleka swala hilo polisi.
Nae Bob Junior alipotafutwa alifunguka kuwa, hakuwahi kujui kuwa binti huyo ana watoto lakini pia hakuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada huyo bali ni video queen pekeake.
Junior aliongeza kuwa kama vp wakutane na jamaa ili awapatanishe tena haitakuwa kazi ngumu kwake kufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment