RnB singer kutoka Marekani
anaetamba sana kwa sasa kwa uimbaji na kucheza kwake, Chris Brown amepata ajali
ya gari jana huko Beverly Hills, Marekani.
Imeripotiwa kuwa, Breezy ambae
alikuwa anaendesha gari yake aina ya Porsche kuelekea kwenye shughuli ya
kujitolea alivamiwa na magari mawili ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakimfuatilia
na ndio inasadikika wamesababisha ajali hiyo.
Paparazzi hao waliokuwa
wakimfuatilia kwa muda mrefu na kutaka kumpiga picha ndio walisababisha gari ya
mwanamuziki huyo kuharibika ingawa Chris Brown [ambae alikuwa mwenyewe kwenye
gari] hakuumia popote.
0 comments:
Post a Comment