Friday, February 1, 2013

diamond platinum



NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’, amewajibu baadhi ya wadau wa muziki wa kizazi kipya ambao wameandika katika mitandao ya kijamii kwamba msanii huyo ameishiwa mistari na anaelekea kuachana na mambo ya muziki.
Akizungumza katika kipindi cha sports extra kinachorushwa na Redio Clouds jijini Dar es Salaam juzi, Diamond alisema Mungu ndiye anayejua mwisho wake na sio binadamu wa kawaida.
“Mungu ndiye anayejua mimi nafanya nini na lini utakuwa mwisho wangu; hao wanaoandika hivyo ni mitazamo yao, mimi siwezi kuwazuia kwani baadhi ya walimwengu huwa hawapendi maendeleo ya wenzao na ndio maana mimi naachia kazi mfululizo ili kuwaziba midomo yao,” alisema Diamond.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...