Mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd hii leo watajaribu bahati
yao ya kusaka nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya ligi ya
mabingwa barani Ulaya pale watakapo pambana na mabingwa wenzao kutoka
nchini Uguriki Olympiakos katika uwanja wa Old Trafford.
Man Utd watajaribu bahati yao, huku wakiwa na kumbu kumbu ya
kukubalia kufungwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa mkondo wa
kwanza, uliowakutanisha na Olympiakos nchini Ugikiri, mwishoni mwa mwezi
uliopita.
Meneja wa klabu ya Man Utd David Moyes amesema pamoja na mwenendo
mbaya kuwaelemea msimu huu bado anaamini kikosi chake kinaweza kufanya
maajabu usiku wa hii leo na kikasonga mbele kwenye michuano hiyo ya
Ulaya.
Wakati huo huo beki wa pembeni kutoka nchini Ufaransa na klabu hiyo
ya Man Utd Patrice Evra amesema anatambua mashabiki wa Man Utd
wameshachoshwa na matokeo mabaya yanayowakabili kwa sasa, lakini hii leo
huenda wakajikuta wakikipongeza kikosi chao kutokana na maandalizi
mazuri waliyo yafanya.
Evra amesema wanatambau wameshafanya makosa ya kukubali kufungwa
katika mchezo wa kwanza dhidi ya Olympiakos lakini wana nafasi nyingine
ya kucheza nyumbani kwa ajili ya kupindua matokeo hayo na kuhakikisha
wanashinda kwa kishindo.
0 comments:
Post a Comment