Mwanamuziki wa kike wa Kenya, Victoria Kimani ameamua kusema na mashabiki wake kwa lugha ya Kiswahili kupitia Instagram.
Mwimbaji huyo wa Chocolate City ambaye alishafanya kazi na wasanii
wakubwa duniani kama Busta Rhymes amezungumzia sakata la kuonekana
katika picha na baadhi ya wasanii wakubwa na kuhusishwa na uhusiano wa
mapenzi. Suala ambalo lilizuka baada ya kupiga picha na Diamond
Platinumz walipokutana Afrika Kusini.
Victoria ameeleza kuwa kupiga picha hakumaanishi kuwa kuna kitu chochote kinachoendelea zaidi ya kazi ya muziki.
Katika hatua nyingine, Victoria ameonesha furaha yake kwa kufanya
kazi ya pamoja na wasani wa Tanzania wanaofanya vizuri kwenye game la
Bongo Flava, Diamond na Ommy Dimpoz akiwa msanii wa kwanza wa kike
kuwakutanisha wakali hao.
Huu ndio ujumbe alioandika Victoria Kimani.
“Mafans wangu wote, nawapenda sana sana. Nafanya kazi ya muziki
kwa bidii na kwa sababu yenu. Nimepiga picha na wanamuziki wengi na
wakubwa sana kote duniani. Na hiyo HAIMAANISHI KUNA MAMBO MENGINE
YANAENDELEA NJE ya KAZI YA MUZIKI. Kwa hayo machache, ninafuraha sana
kufanya kazi na wanamuziki wakubwa zaidi wa Bongo @ommydimpoz na
@diamondplatnumz kwenye single moja. Mimi ndiye msanii wa kwanza wakike
kufanya single moja na hawa wawili. Tunafocus na mambo makubwa zaidi ili
East Africa iende mbele kimuziki. NAWAPENDA WOTE. Mimi wenu VICTORIA
KIMANI .”
0 comments:
Post a Comment