Robin van Persie alifunga mabao matatu na kuisaidia mabingwa watetezi
wa ligi kuu ya Uingereza Manchester United, kujikatia tiketi ya
kushiriki robo fainali ya kombe la kilabu bingwa
barani Ulaya baada ya kuinyuka Olympiakos mabao 3-0 katika mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa Old Trafford.
Mabao hayo ya Van Persie yalinusuru kocha David Moyes shtuma ya
kuiumbua sifa ya ya timu hiyo ambayo imekuwaikishuhudia msururu wa
matokeo duni katika ligi ya nyumbani.
Van Persie alifunga mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa vibaya mda mchache tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Baadaye mshambulizi huyo wa Uholanzi aliongeza bao lingine baada ya
kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambulizi mwenza Wayne Rooney.
Van Persie alisajili bao lake la tatu kupitia mkwaju wa free kick na
kumhakikishia Moyes fursa ya kujiunga na Chelsea katika hatua ya robo
fainali ya mchuano huo wenye kitita kikubwa zaidi barani Uropa.
Licha ya mashambulizi kadhaa Olympiacos kutoka Ugiriki mlinda lango
wa Manchester United David De Gea alilazimika kufanya kazi ya ziada
kuinyima klabu hiyo kutoka Ugiriki bao moja tu la ugeninivan Persie asherekea na Rooney
walilohitaji kusawazisha mambo.
Olympiacos ilishinda mechi ya mkondo wa kwanza mabao 2-0 na ilihitaji
sare ya aina yeyote ama bao moja tu la ugenini ilikufuzu kwa hatua
ijayo kutokana na sheria ya bao la ugenini.
Timu hiyoitajilaumu yenyewe kwani ilpoteza nafasi nyingi tu za kufunga bao hilo muhimu.
Joel Campbell ambaye anaichezea kwa mkopo kutoka Arsenal alimchenga
mlinzi Phil Jones akampigia pasi Hernan Perez ambaye aliboronga na
kuupiga nje.
Kutokana na ushindi huo mkubwa ,Manchester United sasa inajiunga na Chelsea kama wawakilishi wa uingereza katika robo fainali .
Ujerumani inawakilishwa na mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern
Munich na Borussia Dortmund huku Uhispania ikijivunia timu tatu yaani ,
Real Madrid, Athletico Madrid na Barcelona .
Paris Saint Germain ndiyo timu ya pekee kutoka Ufaransa.
Droo ya robo fainali ya mchuano huu itafanyika Ijumaa .
BBC
0 comments:
Post a Comment