Chris Brown ambaye hivi sasa sheria imemshikilia na sio mtu huru,
ameendelea na ratiba yake na kuachia video mpya ya wimbo wake ‘Loyal’
aliowashirikisha Lil Wayne na Tyga.
Video ilishutiwa California
siku chache baada ya kuachiwa kutoka Rehab mwezi February alipokuwa
akipata matibabu ya kudhibiti hasira. Usher ameonekana kwenye video hii
akimpa kampani Chris.
Loyal ni miongoni mwa nyimbo zitakazopatikana kwenye albam yake ‘X’ inayotarajiwa kutoka May 5 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa.
0 comments:
Post a Comment