Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero, pamoja na beki kutoka nchini Serbia Matija Nastasic, wataukosa mchezo wa hii leo ambapo Man City wanavuka mitaa kuelekea Old Trafford, kwa ajili ya kupambana na mabingwa watetezi Man Utd.
Meneja wa klabu ya Man city, Manuel Pellegrini amethibitisha taarifa
za kukosekana kwa wachezaji hao wawili, kutokana na hali zao kiafya
kutoruhusu kujumuika na wenzao kwenye mchezo huo ambao unasubiriwa kwa
hamu kubwa na mashabiki wa soka karibu ulimwenguni kote.
Manuel Pellegrini, amesema kukosekana kwa wachezaji hao hakumaanishi
kama amekatishwa tamaa ya kuendeleza kasumba ya kusaka ushindi dhidi ya
wapinzani wake kama alivyofanya wakati wa mchezo wa mzunguuko wa kwanza
ambapo Man Utd walikubali kichapo cha mabao manne kwa moja.
Amesema pamoja na kuweka matarajio hayo bado wanakwenda katika uwanja
wa ugenini huku wakiwa na tahadhari ya kutambua wapinznai wao
watahitaji kucheza kwa kutaka kulipiza kisasi.
Hata hivyo Manuel Pellegrini amezungumzia mbio za ubingwa kwa kusema
kwake hazipi nafasi kubwa katika kipindi hiki, zaidi ya kutazama mchezo
mmoja baada ya mwingine akianzia mchezo wa hii leo na kisha mchezo ujao
dhidi ya Arsenal mwishoni mwa juma hili.
Amesema ni muhimu kwa sasa kuangalia sana suala la ushindi, kwani
hajui ni point ngapi ambazo kikosi chake kinatakiwa kufikisha ili
kukamilisha azma ya kutwaa ubingwa, zaidi ya kuzipa kipaumbele point
tatu muhimu.
Wakati huo huo meneja wa klabu ya Man Utd David Moyes, amesema hana
shaka na mpambano hii leo dhidi ya Man city, kutokana na kikosi chake
kuanza kurejea katika hali ya kujiamini kama kilivyoonekana katika
michezo miwili iliyopita.
Amesema kikosi chake kitakwenda katika uwanja wa nyumbani hii leo
lengo likiwa ni moja tu, la kusaka ushindi ambao utawaongezea point tatu
muhimu.
Michezo mingine ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza itakayochezwa hii leo:
Newcastle Utd Vs Everton
Arsenal Vs Swansea City
0 comments:
Post a Comment